Faragha
Faragha na taarifa zako
Imesasishwa 10/11/2026
Tunachukua taarifa chache tu tunazohitaji kukuhudumia, na hatuziuzi wala kuzitoa kwa ajili ya matangazo.
Tovuti hii
- Haina vidakuzi (cookies) vya matangazo wala ufuatiliaji. Inahifadhi lugha uliyochagua tu (kidakuzi kimoja, “zebra_lang”).
- Tunahesabu vitendo vichache bila kukutambua: kufungua menyu, kubonyeza njia, simu, WhatsApp au kupakua app. Tunahifadhi idadi kwa siku tu, si anwani ya IP wala kitambulisho.
- Ramani ya OpenStreetMap kwenye ukurasa wa Tembelea inapakiwa ukibonyeza tu. Viungo vya Google Maps, WhatsApp na Instagram vinakupeleka kwenye huduma hizo, ambazo zina sera zao.
- Hatuchukui oda wala malipo kupitia tovuti.
Ukiagiza mgahawani, kwa simu au WhatsApp
Tunaandika chakula, jina, na kwa delivery namba ya simu na mahali pa kuletewa, ili kuandaa na kukuletea oda na kutoa risiti. Ujumbe wa WhatsApp unatumika kukujibu kuhusu oda hiyo; hatutumi matangazo bila ridhaa yako. Andika STOP na hatutakutumia ujumbe tena.
Muda tunaohifadhi
Rekodi za mauzo na risiti huhifadhiwa kwa muda unaotakiwa na sheria za kodi. Taarifa nyingine tunaziondoa zisipohitajika tena.
Haki zako
Unaweza kuomba kuona, kusahihisha au kufuta taarifa zako kwa kupiga 0688 151 783 au kutuandikia WhatsApp.